Skale hakuwa na sehemu ya kuishi, Alilala kwenye gari

Skale hakuwa na sehemu ya kuishi, Alilala kwenye gari

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Skales ambaye alitamba miaka ya nyuma kwa wimbo wake “Shake Body”, ameweka wazi maisha yenye changamoto aliyopitia kipindi baada ya kuachana na label yake ya EME iliyokuwa ikimsimamia.

Skale ameeleza kuwa baada ya kutemana na label yake, ilimtaka aache kila kitu kuanzia nyumba aliyokuwa akiishi, kwani ilikuwa ikimilikiwa na label hiyo, zaidi alichobaki nacho ilikuwa gari alilonunua kwa pesa zake.

Kutokana na kukosa sehemu ya kuishi ilimbidi alale kwenye gari  lake hilo, wakati huo akiwa bado hajaachia “shake body”,  Skales amesema kujua kuwa wimbo huo uliopo kwenye flash yake ndiyo utakuja kubadilisha maisha yake.

Aliachia “shake body” akiwa hana pesa ya kuufanyia matangazo akauweka kwenye Sound Cloud  alishangaa wimbo huo ulipenya kila kona na kumbadilishia maisha yake upya.

Shake Body ulitoka miaka 9 iliyopita hadi sasa umetazamwa na watu milioni 39 kwenye mtandao wa Youtube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags