Sita wakamatwa mauji ya beki wa Kaizer Chiefs

Sita wakamatwa mauji ya beki wa Kaizer Chiefs

Watu sita wanadaiwa kuhusika katika kifo cha aliyekuwa mchezaji wa ‘klabu’ ya #KaizerChiefs, #LukeFleurs wamekamatwa na Polisi nchini Afrika Kusini jana Jumatano April 10.

 Inaelezwa kuwa washukiwa hao wamekamatwa katika kitongoji cha Soweto, kusini Magharibi mwa jiji hilo baada ya kugundulika wanahusika kwa wizi wa gari la Fleurs.

Wachunguzi katika kesi hiyo wanadai kuwa washukiwa hao ni sehemu ya kundi la uhalifu linalohusika na wizi mwingine wa magari huko Gauteng.

Luke Fleurs (24) alifariki kwa kupigwa risasi wiki iliyopita alipokuwa akijaza mafuta katika moja ya kituo cha mafuta kilichopo jijini Johannesburg.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags