Sita wadakwa kifo cha AKA

Sita wadakwa kifo cha AKA

Baada ya uchunguzi kufanyika kwa takribani mwaka kufuatiwa na kifo cha ‘rapa’ AKA hatimaye polisi nchini Africa Kusini imetoa taarifa ya kuwakamata watu sita ambao wamehusika na mauaji hayo.

Taarifa hiyo imetolewa na jeshi la polisi nchini humo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika siku ya jana Februari 27.

Akitoa taarifa hiyo kiogozi wa polisi Bheki Cele amesema kuwa watu sita wamekamatwa na watafikishwa mahakamani siku ya Alhamis Februari 29, huku akiweka wazi kuwa mshukiwa mkuu ana umri wa miaka 36 na huenda wengine wakaongezeka.

Kiernan Forbes, maarufu kama AKA alifariki kwa kupigwa risasi Februari 10 mwaka jana nje ya mgahawa wa Durban, Afrika Kusini.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags