Sio kinyonge Roma aonesha chati zake na rapa wa Marekani

Sio kinyonge Roma aonesha chati zake na rapa wa Marekani

Mkali wa muziki wa Hip-hop kutoka Bongo Roma Mkatoliki ameonesha mazungumzo yake na ‘rapa’ kutoka Marekani Jadakiss, kwa lengo lake likiwa ni kufanya naye kazi.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Roma ame-share chati zake na msanii huyo zikionesha Jada alivyomtafuta Roma huku akisubiri ajibu ‘meseji’ zake kwa ajili ya kuanza taratibu za kufanya kazi pamoja.



‘Rapa’ Jadakiss amewaku kufanya ngoma na mastaa mbalimbali Marekani akiwemo Rick Ross, Fat Joe, Meek Mill, Dj Khalied na wengineo.

Roma ame-share chati hizo ikiwa ni muda mchache tuu kupita tangu mwanamuziki Diamond ku-share chati zake na Jason Derulo akiomba kufanya naye ngoma, lakini pia wakati huo huo kionjo cha wimbo wa pamoja wa Diamond na Swae Lee kikiwa tayari kimeshatoka.

Endapo ‘kolabo’ hizo zitafanikiwa basi wasanii hao wa Bongo Fleva watakuwa wamekata kiu yao kwa kiasi flani katika kuupeleka muziki huo kimataifa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags