Sio Diamond tu hadi Burnaboy ana-copy nyimbo

Sio Diamond tu hadi Burnaboy ana-copy nyimbo

Kama ni mtu wa mitandao utakuwa umekutana na story za #diamondplatnumz ku-copy nyimbo za wanamziki kutoka nje ya nchii hasa nyimbo za wasanii kutoka Nigeria.

Na siku chache nyuma  #Diamondplatnumz alijikuta kwenye lawama kuhusiana na wimbo wa "Enjoy" aliyoshirikishwa na  #Jux, kudaiwa kuwa kwenye wimbo huo  ka-copy baadhi ya vitu kutoka kwenye wimbo wa Spyro  ‘who is your guy’.

Tuhuma hizo zilipelekea baadhi ya wadau wa muziki na wasanii akiwemo Spyro kumtetea mwanamuziki huyo na kusema kuwa ni kawaida kwa wasanii ku-copy nyimbo kwani hakuna mtu mwenye chake.

Mchezo huo wa kucopy si tu kwa #Diamond bali  umejidhihilisha pia kutoka  kwa mwanamuziki  Burna Boy kwenye wimbo uitwao  #Temper wa mwaka 2017  aliyoshirikishwa na Skales , ulikuwa ni copy ya wimbo wa ‘Tears and blood’ ulioimbwa na Fela Kuti mwaka 1997.

Wimbo mwingine wa mkali huyo  ni  #Ye ambao ali-copy kutoka kwenye  wimbo huohuo wa Treas and blood huku wimbo mwingine alio-copy ni #Anybody ambao original yake ni ngoma ya ‘We we’ kutoka kwa  mwanadada Angelique Kidjo wa mwaka 1992, kubwa kuliko ni hii ya Last Last ambayo original yake ni wimbo wa Toni Braxton wenye jina ya ‘He wasn’t man enough’ wa mwaka 2000.

Kwa upande wa Burnaboy kupitia mahojiano aliyofanya na #PodCast iitwayo Stop One Distribution,  alieleza kuwa yeye ha-copy ila ana-sample beat na baadhi ya maneno huku akiongezea ubunifu na kisha kutoa kitu kipya lakini pia anaingia makubaliano na wamiliki na hata kulipa asilimia kadhaa za mapato kwa nyimbo alizo-copy.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags