Sintofahamu Bony Mwaitege akihusishwa kufariki ajalini

Sintofahamu Bony Mwaitege akihusishwa kufariki ajalini

Kutokana na taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa mwanamuziki wa nyimbo za Injili nchini, Bony Mwaitege amefariki dunia, Seme Shitindi ambaye ni mtu wa karibu wa familia ya mwimbaji huyo na mshirika wake katika Kanisa la Safina, amekanusha taarifa hizo akisema ni za uzushi.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu Julai 22, 2024, Shitindi amesema muda si mrefu amezungumza kwa simu na mwimbaji huyo.

"Ni uongo, Mwaitege ameingia asubuhi hapa alikuwa Mbeya, sasa hivi yupo nyumbani kwake wala hajafariki. Jana alikuwa anamaliza mkutano Tunduma, wala hakuwepo Kenya, hivi sasa nilikuwa naongea naye," amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Waimbaji wa Nyimbo za Injili Tanzania, Ado Novemba amesema hana taarifa kamili kuhusu suala hilo, kwani juhudi zake za kumtafuta Bony zimegonga mwamba kwa simu kutopokelewa.

"Tunafuatilia lakini hatujapata majibu sahihi kwa sababu na sisi tumesikia tu, nimejaribu kumpigia simu zake hazijapokelewa," amesema Ado.

Hata Mwananchi ilipojaribu kumtafuta mwimbaji huyo simu yake iliita bila kupokelewa.

Utakumbuka kuwa mwimbaji huyo amewahi kutamba na nyimbo kama vile Safari Bado, Dunia Dunia, Acha Nizaliwe, Bado Nampenda, Mke Mwema, Sisi Sote, Imba, Mama na Neema Imenibeba na nyingine.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags