Singida Big Star sasa itaitwa Singida Fauntain Gate FC

Singida Big Star sasa itaitwa Singida Fauntain Gate FC

Mjumbe wa Bodi ya Singida Fountain Gate FC, John Kadutu amesema timu ya Singida Big Stars ambayo ilimaliza nafasi ya nne msimu wa 2022/23 na kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika imeinunuliwa na timu Fountain Gate yenye maskani yake Dodoma.

Singida Big Stars kuanzia leo Juni 14 itajulikana kama Singida Fountain Gate FC.

Pia timu ya Fountain Gate Princess itakuwa timu ya Wanawake ya Singida Fountain Gate FC ili kukidhi matakwa ya CAF timu zinazoshiriki michuano ya kimataifa msimu ujao kuwa na timu ya wanawake.

Uongozi wa timu hiyo umetangaza hilo leo ukizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags