Singeli ya wivu yamfanya Ibrah ahame upande

Singeli ya wivu yamfanya Ibrah ahame upande

Baada ya singeli inayotamba Ndani na Nje ya Tanzania ya ‘Wivu’ kufanya vizuri katika platform zote, mwanamuziki wa Bongo Fleva Ibrah Tz ameamua kuwa atawekeza zaidi kwenye muziki huo kutokana na watu kumpokea vizuri.

Ibrah ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ameshare kipande cha ‘Wivu Remix’ video akieleza kuwa kutokana na kupokelewa kwa ukubwa basi ameamua kuwekeza nguvu nyingi katika Singeli huku akiwataka wasanii wa singeli kumuacha kidogo mwaka 2025.

“Nimenyoosha mikono juu huu wimbo umenifanya niamini kuwa wa tanzanian 🇹🇿 tunapenda sana music wetu wa singeli na ahadi yangu nitazidi kuwekeza zaidi kwenye music wa singeli 2025 kauli mbio yetu itakuwa ni singli kwanza wasanii wasingeli acheni utani na kazi yangu,” ameandika Chinga

Aidha baada ya kutoa kauli hiyo baadhi ya mashabiki kupitia chapisho hilo wamempongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya na kuufanya wimbo huo kuwa bora zaidi.

Mpaka kufikia sasa ‘WIVU Remix’ unazaidi ya watazamaji 866,690 kupitia mtandao wa Youtube huku wimbo huo ukiwashirikisha wasanii kama Dj Mushizo, Ibraah, Jay Combat na Baddest 47.

Hii ni singeli ya pili kwa Ibrah kushirikishwa na kufanya vizuri, Utakumbuka kuwa mwaka 2021 alishirikishwa katika singeli ya ‘Do Lemi go’ na Kinata Mc, ambapo mpaka kufikia sasa inazaidi ya watazamaji milioni mbili katika mtandao wa YouTube.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags