Simba yafanya jaribio la kumng’oa Maxi Yanga

Simba yafanya jaribio la kumng’oa Maxi Yanga

‘Klabu’ ya Simba wamefanya jaribio zito la kutaka kumng’oa juu kwa juu kiungo wa Yanga Mkongomani, Maxi Nzengeli ambaye alipiga mabao mawili dhidi ya Simba kwenye ushindi wa mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu Bara hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti imeeleza kuwa Simba wamepiga simu kwa ‘Klabu’ ya zamani ya Nzengeli, Union Maniema ya DR Congo na kumwaga ‘ofa’ nzito wakijua kwamba huenda kiungo huyo yuko Jangwani kwa mkopo kama ilivyowahi kuzushwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya wachambuzi.

Hata hivyo, Mwanaspoti inajua kuwa Simba wamejibiwa Nzengeli ni mali halali ya Yanga na kama kuna hatua za kumuuza basi ‘klabu’ ya Maniema watapata mgao wao lakini watu wa kwanza watakao simamia biashara hiyo ni Wanajangwani.

Wanamsimbazi hawakuridhika wakaingia mfukoni na kutoa ahadi nzito mabosi hao wa klabu ya Maniema wakiweza kumchomoa Maxi Yanga watamwagiwa fedha mara mbili walizopewa na Yanga.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags