Simba vs Usgn kuchezwa saa 4 usiku

Simba vs Usgn kuchezwa saa 4 usiku

Mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho barani Afrika kati ya Simba SC ya Tanzania dhidi ya US Gendermarie ya Niger, utachezwa Jumapili saa 4:00 usiku badala ya saa 1:00 usiku.

Hii imekuja  baada ya makubaliano na shirikisho la soka barani afrika CAF ili kwenda sawa na mchezo mwingine wa kundi hilo.

Simba SC inahitaji ushindi siku ya Jumapili dhidi ya USGN ili kujihakikishia nafasi ya kufuzu robo fainali kombe la shirikisho.

Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally amethibitisha mabadiliko ya muda wa mchezo huo alipokuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari.

Sababu ya mabadiliko ya muda huo ni kwamba michezo yote ya kundi hilo ichezwa muda mmoja ambapo siku hiyo RS Berkane nao watakuwa wanacheza na ASEC Mimosas.

''Tumekubaliana na wenzetu wa CAF sambamba na ASEC, Berkane na Us Gendermarie kuupelekea mchezo wetu kuchezwa saa nne kamili usiku kwa maslahi mapana ya mchezo wa soka "amesema Ahmed Ally .






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags