Simba Sc , Waifata Orlando Pirates kwa Madiba

Simba Sc , Waifata Orlando Pirates kwa Madiba

Ebwana eeh!!Klabu ya Simba  imeondoka Dar es salaam leo asubuhi na mapema   Kuelekea nchini Afrika Kusini ambako itacheza mchezo wa robo fainali wa mkondo wa pili ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Orlando Pirates.

Aidha timu ya Simba Sc ambao ni wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye michuano ya vilabu barani Afrika wanaelekea kwenye mchezo huu wakiwa na faida ya kuongoza bao 1-0. Ushindi ambao walipata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Aprili 17, 2022.

Ushindi huo uliopatiakana  katika dimba la Benjamini mkapa Dar es salaam bao pekee ambalo lilifungwa na Shomari Kapombe kwa kwaju wa penati.

Kikosi cha Simba kimeondoka leo ikiwa tayari kwa mchezo huo wa mkondo wa pili utakaochezwa katika dimba la Orlando jiji Johannesburg.

 

Hata hivyo Simba itahitaji matokeo ya sare yoyote ile au ushindi ili kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hii.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags