Shilole: Ninafanya makusudi kuongea kingereza

Shilole: Ninafanya makusudi kuongea kingereza

Msanii wa filamu na muziki wa kizazi kipya, Shilole amesema kukosea kwake kuzungumza Kiingereza huwa anafanya makusudi ili watu wacheke.

Shilole anayejishughulisha pia na biashara ya kuuza vyakula amekuwa akionekana mara kadhaa akizungumza Kiingereza kwa kuchapia na kuna baadhi ya mashabiki wamekuwa wakimponda kwa kumtaka aendelee na kuzingumza Kiswahili tu kuliko kulazimisha lugha za watu, lakini ameamua kuwajibu.

Akizungumza na Mwanaspoti juzi usiku kwenye sherehe ya mchekezaji Jacob William ‘Ringo’ a.k.a Mkweche, mwanadada huyo alisema yeye ni mchekeshaji, japo amekuwa akiigiza filamu akiwa siriazi kwa kuwa ni sehemu pia ya kazi yake .

Shilole alisema anapenda sana fani ya uchekeshaji na ndio maana huwa anapaenda kuzingumza Kiingereza cha kuchanganya maneno ili kuchekesha.

“Mimi ni mchekeshaji unajua na huwa napenda kuona watu wanacheka nikiwa naongea. Ndio maana huwa naongea Kiingereza kisichoeleweka ili watu wacheke tu, kwani ndio furaha yangu,” alisema.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags