Shilole kurudi gym

Shilole Kurudi Gym

Aiseee kimeumana!! unaambiwa baada ya comments nyingi za mashabiki mitandaoni kumtaka  msanii wa muziki na Filamu Zuwena Mohamed maarufu kama  Shilole apunguze mwili wake huenda ikawa  amezikubali.

 Star  huyo, kwani sasa hivi anatafuta mwalimu wa mazoezi na yupo njiani kurudi gym.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Shilole ametoa taarifa hiyo kwa kupost picha yake ya zamani kabla hajakuwa na mwili mkubwa kisha akaandika maneno haya.

"Je umemjua huyo binti hapo, kama ndio basi kakubali kurudi gym na anataka traina wa kumfata kwake malipo sio shida, kikubwa mazoezi yawe standard sio kokomoana maana walimu wengine khaaaaa"

Niambie mdau unaonaje hapo abaki vilevile alivyo sasa au arudi kuwa shishi wa enzi zileee?tupia comment yako hapo kupitia www.mwananchi scoop.co.tz.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post