Sherehe za Halloween, lengo kuwakumbuka marehemu

Sherehe za Halloween, lengo kuwakumbuka marehemu

Ukiwa mtu wa mitandao lazima utakuwa umekutana na picha au video za kutisha zikiwahusisha baadhi ya watu wakiwemo mastaa mbalimbali wakiwa kwenye mionekano ya ajabu. Kawaida picha na video hizo zinahusisha sikukuu inayofahamika kama Halloween, inayoadhimishwa kila ifikapo Oktoba 31.

Sikukuu hiyo imekuwepo kwa zaidi ya miaka elfu moja, awali ilikuwa ya kidini lakini baada ya karne kadhaa kupita ikiwa ya kidunia huku lengo kuu likiwa kuwakumbuka marehemu.

Sherehe hii mara nyingi imekuwa ikifanyika Ulaya na Amerika Kaskazini, ikiadhimishwa kwa kuvalia mavazi ya kutisha, jack-o’-lanterns, kuchonga maboga pamoja na kujiweka kama mfu.

Sikukuu hii pia inaashiria mwanzo wa Allhallowtide, kipindi cha siku tatu cha Kikristo kinachoelekezwa kwa kuwakumbuka marehemu, ambacho huanza na Halloween (Oktoba 31) na kufuatiwa na Siku ya Watakatifu wote (Novemba 1) na Siku ya wote Waliofariki (Novemba 2).

Licha ya kupigwa vita kwa takribani miongo kadhaa lakini kwa sasa sherehe ya Halloween imekuwa kubwa haswa kwa watu wa Marekani huku wakiiadhimisha kwa kufunga mitaa na barabara na kuvalia mavazi mithili ya zombie.

Kwa mwaka 2024 sherehe hizo zimezidi kupamba moto na kuwateka mastaa kutoka katika tasnia mbalimbali Marekani wakiadhimisha kwa kuvalia mavazi yanayotakiwa wakiwemo Fatjoe, Halle Bailey, Jonathan Majors na wengineo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags