Sheikh Kishki:Tutalipa mahari kwa vijana 50

Sheikh Kishki:Tutalipa mahari kwa vijana 50

Taasisi ya Dini ya Kiislam ya Al- Hikma Foundation kutoka Jijini Dar es salaam, imetanganza kuwaozesha vijana 50 kwa kuwalipia mahari ambao bado hawajaoa kutokana na changamoto za kifedha na wapo tayari kutekeleza ibada hiyo ya ndoa.

Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh Nurdini Kishki ameleeza hayo jana wakati wa Mashindano ya 23 ya kimataifa ya kuhifadhi Qur’aan tukufu, uwanja wa Uhuru Dar es salaam.

Yakihudhuriwa na viongozi wa Serikali na Kidini huku Mgeni rasmi katika mashindano hayo akiwa ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dkt. Hussein Ali Mwinyi.

Aidha Sheikh Kishki amenukuliwa akisema “Tutafanya ndoa ya pamoja kwa watu 50, mahari ya vijana hao itakuwa juu yetu sisi Al- Hikma Foundation, sharti usiwe unaongeza mke wa pili na ndoa itafanyika Dar es salaam chini ya Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags