Shangwe la mashabiki baada ya Celine kupanda jukwaani

Shangwe la mashabiki baada ya Celine kupanda jukwaani

Baada ya dada wa mwanamuziki maarufu kutoka nchini Marekani Celine Dion, Claudette Dion kutoa taarifa mpya kuhusiana maendeleo ya mwanamuziki huyo Desemba mwaka jana, kwa kuweka wazi kuwa Celine anasumbuliwa na matatizo ya misuli na huenda asirudi tena jukwaani kutokana na maumivu , hatimaye Celine ameonekana tena kwenye Tuzo za Grammy zilizokuwa zikitolewa usiku wa kuamkia leo akiwa anazidi kuimarika kiafya.

Celine alipanda jukwaani kwenda kumtaja na kumkabidhi mshindi wa tuzo  katika kipengele cha ‘Album of the year’ tuzo hiyo iliyoenda kwa mwanadada Taylor Swift.

Celine alipokelewa kwa shangwe baada ya kupanda jukwaani hapo kutokana na kuonekana akiwa na afya nzuri, huku baadhi na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii wakieleza kuwa huenda kukawa na matumaini ya kumuona tena jukwaani kwa siku zijazo.

Ikumbukwe kuwa Celine Dion aliweka wazi ungonjwa unaomsumbua wa ‘Stiff-Person Syndrome’ Desemba 2022 kupitia ukurasa wake wa Instagram na kulazimika ku-cancel matamsha yote aliyopanga kuyafanya mwaka 2023.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags