Shangazi mtu akakinukisha na kusema haolewi mtu hapa...

Shangazi mtu akakinukisha na kusema haolewi mtu hapa...

Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2004 nilipata kibarua cha muda wilayani Kilindi katika mji wa Songe yalipo makao makuu ya wilaya hiyo ambayo kwa wakati huo ilikuwa ndiyo wilaya mpya baada ya kumegwa kutoka wilaya ya Handeni. Hii ilitokea Mahsusi ili kusogeza huduma za kijamii kwa wananchi kwa sababu kulikuwa na umbali wa takriban kilomita 70 kutoka Handeni mpaka mji wa Songe.

Baada ya kumaliza chuo nilisota kwa muda wa takriban mwaka mmoja na ndipo Rafiki yangu ambaye baba yake alikuwa na kampuni yake ya ujenzi akanisaidia kupata kibarua kwenye kampuni ya baba yake na kupelekwa kusimamia ujenzi wa kupanua zahanati iliyoko katika wilaya hiyo ya Kilindi ili iwe na hadhi ya Hospitali ya Wilaya.

Kiukweli sikusomea mambo ya ujenzi lakini kwa kuwa nimesoma kidogo baba wa Rafiki yangu aliona nikamsaidie kusimamamia ujenzi kule Songe hususan upande wa stoo na manunuzi ya vifaa vya ujenzi. Nilipofika mjini Songe awali nilifikia nyumba ya wageni yaani Guest House na baada ya mwezi nilishauriwa na Boss wangu nitafute Nyumba ya kupanga ili kupunguza gharama.

Nilibahatika kupata nyumba ya mama mmoja  wa makamo hivi mjane na alikuwa na umbo dogo kiasi cha kumfanya kuonekana kama umri haujaenda. Huyu Mama alikuwa ni kutoka kabila la Wazigua na alikuwa ameolewa na mumewe Mzigua mwenzie ambaye alihamia Songe kutoka Handeni kibiashara na kulowea Songe hadi alipofariki kwa ajali ya pikipiki akitokea Mnadani kwenye biashara zake.

Kwa msiojua Songe ni mji ambao linapatikana kabila la Wanguu ambalo lugha yao inaingiliana na Kizigua na Kikaguru na Kisambaa kidogo kama sikosei. Hawa ndiyo wenyeji wa mji huo au wilaya ya Kilindi kwa ujumla.

Kwa kuwa yule bwana alikuwa ameshajijenga Mkewe aliendelea kubaki pale akiendelea na biashara alizoacha mumewe. Alikuwa na Watoto wawili wa kike na wa kiume ambao wakati nahamia kwenye nyumba ile niliambiwa wote wanasoma sekondari huko Tanga shule za bweni.

Kwa kipindi kifupi nilipohamia pale yule mama mwenye nyumba yangu ambaye alikuwa ni mweupe mfupi na mwembamba mwenye umbo la kuvutia hasa alianza vituko vyake ambavyo vilinifanya nihisi kama vile ananitaka kimapenzi. Alianza kuniwekea chakula na usiku ananiita tuangalie movie Ndani kwake kwa sababu alidai anakuwa bored akiwa peke yake.

Vituko vyake vilikuwa vingi ikiwa ni Pamoja na kunivalia kanga nyepesi huku akiwa mtupu na kuacha mapaja wazi wakati tukiangalia movie sebuleni kwake. Hali hiyo ilinifanya nishindwe kujizuia tukajikuta tukianza mahusiano ya kimapenzi na mama mwenye nyumba wangu. Kuanzia hapo tukawa tunaishi pika pakua kama  mume na mke. Japo tulificha kwa sababu nyumba ilikuwa na ukuta na geti na alikuwa na mfanyakazi mmoja binti aliyekuwa akimsaidia kuuza duka na alikuwa anakuja na kuondoka siri ya mahusiano yetu haikuvuja mapema lakini hata hivyo baadaye ilikuja kujulikana hivyo na wambea japo tuliendelea kuficha ficha.

Kwa upande wa Watoto wake, walipokuwa wanakuja likizo tulikuwa tunaishi kila mtu chumbani kwake na walitambulishwa kwangu kuwa ni mpangaji na wakaambiwa waniite mjomba. Kwa bahati wale wanae walinipenda sana hasa kwa sababu nilikuwa nawafundisha masomo ya jioni nikawa nimejijengea ukaribu na ile familia kwa ujumla. Hata hivyo Pamoja na uwepo wa wanae lakini bado tulikuwa tunaendelea na uhusiano wetu kwa kujiiba bila wao kujua, ingawa nadhani hata wao walihisi

Kule kazini nilikuwa naendelea na kazi vizuri na baada ya mwaka mmoja kazi ile ya upanuzi wa hospitali awamu ya kwanza iliisha ikabidi tufungashe kurudi Dar es salaam ili kusubiri mwaka wa fedha kama fungu la bajeti likitoka turudi kuendelea na awamu yapili na ya mwisho ya upanuzi wa hospitali hiyo.

Nilimuaga yule mama mwenye nyumba wangu na mpenzi wangu kwa huzuni sana lakini nilimuahidi nitakuwa nakuja mara kwa mara kumsalimia. Ukweli ni kwamba yule mama alikuwa ananipenda hasa na alikuwa amezama kwenye penzi zito sana kwangu. Ingawa alikuwa amenizidi kidogo kwa umri lakini alikuwa anajiweka kisichana kiasi kwamba inaweza kukuwia vigumu kukisia umri wake. Hata Watoto wake ukiwaoana unaweza kukataa kama siyo wakwake kwa sababu ya umbo lake. Hata hivyo nilikuja kugundua aliolewa mapema sana akiwa na umri wa miaka 16 akiwa bado binti kigori kabisa na akawahi kuzaa.

Alinisihi sana tuoane tuishi Pamoja pale kwake kwa sababu ule mji ni wakwake baada ya kushinda kesi ya mirathi ya mumewe na kunihakikishia kabisa kuwa sitabughuziwa lakini nilimuomba nirudi kwanza Dar es salaam halafu nikishakuwa tayari kwa jambo hilo la ndoa nitamjulisha.

Nilirudi Dar es salaam na kuendelea na Maisha, tuliendelea na mawasiliano ya mara kwa mara lakini baada ya mwezi mmoja tangu niondoke Songe yule mama mwenye nyumba wangu na mpenzi wangu akanipigia simu na kunipa taarifa za kushtua sana. Aliniambia kwamba anao ujauzito wangu. Nilishtuka kwa sababu nilipomshauri kuhusu kutumia kinga au dawa za uzazi wa mpango aliniambia kwamba hawezi kupata ujauzito tena kwa sababu baada ya kupata mtoto wake wa pili alijitahidi sana kutafuta mtoto mwingine bila mafanikio Pamoja na kutumia dawa nyingi za hospitali na za miti shamba hadi mumewe anafariki hakuwahi kupata ujauzito. Ukweli ni kwamba alikuwa umri wa miaka 35 wakati huo na niliamni kwamba asingeweza kupata ujauzito baada ya kunieleza tatizo lake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Mzee Mtambuzi

A freelance Journalist and also teaching self-empowerment, positive thinking as a means of creating the life you desire including spirituality. He is writing in Mwananchi Scoop every Wednesday Visa na Mikasa.


Latest Post