Shakira kutumbuiza fainali ya Copa America 2024

Shakira kutumbuiza fainali ya Copa America 2024

Mwanamuziki mkongwe wa Colombia, Shakira amethibitishwa kutumbuiza kwenye fainali ya Copa America 2024, siku ya Jumapili inayotarajiwa kuhudhuriwa na mashabiki 54,000.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sky Sport imeeleza kuwa msanii huyo atatumbuiza wakati wa mapumziko ya fainali ya onesho kwenye Uwanja wa Hard Rock huko Miami Gardens, Florida, Julay 14 mwaka huu.

Pia kwa upande wanamuziki huyo amedai kuwa anauhakika kwamba uchezaji wake katika Copa América USA 2024 utaongeza ujumbe wa shauku na umoja wenye afya kupitia michezo.

Utakumbuka Shakira mwenye umri wa miaka 47 aliwahi kutumbuiza katika sherehe za kimataifa kama vile Super Bowl na Kombe la Dunia tatu.

Fainali ya Copa America ya 2024 itakuwa kati ya washindi wa mchezo wa nusu fainali ambapo tayari  timu ya Argentina imeitoa timu ya Canada siku ya jana kwa ushindi wa mabao 2-0 na mpambano mwingine wa nusu fainali ambao unachezwa leo (Uruguay vs Colombia).
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags