Shakira ajengewa sanamu Colombia

Shakira ajengewa sanamu Colombia

Mwanamuziki kutoka nchini Colombia Shakira ajengewa sanamu katika mji wa Barranquilla ambako ndiko aliyozaliwa.

Kupitia ukurasa wa Instagram wa Shakira ame-share picha na video za familia yake wakiwa katika sanamu hilo na kutoa shukurani zake za dhati kwa Taifa hilo na Meya wa Barranquilla, kwa kuthamini anachofanya.

Sanamu hilo lenye urefu wa futi 21 limetengenezwa na Yino Márques kwa kutumia picha iliyopo kwenye ngoma ya Shakira ya "Hips Dont Lie" iliyotoka mwaka 2005.

Hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kujengewa sanamu katika nchi aliyozaliwa, mwaka 2006 Shakira alitengenezewa sanamu la chuma lililosimikwa Metropolitan Park lenye urefu wa futi 16.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags