Shabiki atolewa uwanjani kwa kumbagua Vinicius

Shabiki atolewa uwanjani kwa kumbagua Vinicius

Mchezaji wa ‘klabu’ ya #RealMadrid, Vinicius Junior ametoa pongezi kwa ‘klabu’ ya #Sevilla kwa kuchukua hatua za haraka za kumtoa uwanjani na ‘kumripoti’ kwa mamlaka shabiki, baada ya kudaiwa kumtusi na kumbagua mchezaji Vinicius.

Kwa mujibu wa The Sun Sport inaeleza kuwa tukio hilo limetokea katika mechi ya Sevilla dhidi ya Real Madrid, na kumalizika kwa sare ya 1-1 inadaiwa kuwa kuna shabiki alionekana uwanjani akimtolea matusi na ubaguzi wa rangi mchezaji huyo.

Mchezo huyo wa ‘Ligi’ kuu ya Uhispania ‘#LaLiga’ ambao umechezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa ‘klabu’ ya Sevilla, uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan.

Ikumbukwe kuwa mchezaji huyo ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita, amekuwa mwathirika wa matukio 7 ya ubaguzi wa rangi kutoka mashabiki wa ‘timu’ mbalimbali za Uispania.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags