Said ambaye kwa sasa ameweka picha hiyo kwenye billboard mkoani Dodoma, ameiambia Mwananchi kwa watu wanaodai ni rahisi kufanya hivyo wachukue na wao picha zao wakaweke kwenye mabango kama wataweza.
"Siyo bango tu mimi nataweka kila kitu kinachoweza kufanyika kupitia picha. Nilimwambia Ndaro nataka niweke bango akawa anacheka haamini. Akaamka Jumatatu akakuta watu wanaposti billboard alijua nazingua.
"Dodoma ni makao makuu anatokea Rais lakini pia kuna ex wangu kwa hiyo nimemwekea kule alipo. Mkianza kulizoea la Dodoma mkalichukulia kawaida nawawekea pale Morocco kazi yangu ni kila mnapoanza kuzoea nawapiga na kitu kizito,"amesema.

Amesema ametumia Sh7 milioni kuweka bango hilo ikiwa ni baada ya gharama za kuweka Dar kuambiwa ni Sh9 milioni.
"Hilo ni mwanzo tu litakaa kwa mwezi mzima. Kabla halijashushwa nawawekea lingine. Ile picha imefanya kampuni nyingi kuniamini. Mimi ni mchekeshaji ambaye kwa sasa nakataa shoo maana ni nyingi ile ni moja ya picha ya thamani sana kwangu.
"Kwenye page yangu ya Instagram zipo tatu na mpango wa kuishusha ya Mwamposa niweke ya Hussein Ali Mwinyi ( Rais wa Zanzibar), kudumisha muungano. Sasa hivi nina mpango wa kufanya shoo zangu. Nina shoo ya tofauti sana bungeni nasubiri kupewa ratiba na Madame Tulia ( Spika wa Bunge Tulia Ackson), hiyo imetokana na picha na perfomance yangu ya siku ile ya tuzo,"amesema.
Utakumbuka picha aliyoweka Said kwenye bango ni ile aliyopiga na Rais Samia kwenye usiku wa tuzo za vichekesho zilizofanyika Februari 22, 2025 jijini Dar es Salaam.
Leave a Reply