Serikali yapiga marufuku vitabu 16  vya watoto

Serikali yapiga marufuku vitabu 16 vya watoto

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda  amepiga marufuku vitabu 16 vya watoto kutumika shuleni kwa madai ya kutetea haki za wapenzi wa jinsia moja LGBTQ.

Mfululizo wa Diary of a Wimpy Kid unasemekana kukiuka mila, desturi na tamaduni za nchi.

Shule zinazotumia vitabu hivyo zitachukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria, ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili wao.

Vitabu vilivyopigwa marufuku ni Diary of a Wimpy Kid: Rodrick Rules, Diary of a Wimpy Kid: The Last Straw, Diary of a Wimpy Kid: The Ugly Truth, Diary of a Wimpy Kid: Cabin Fever, Diary of a Wimpy Kid: The Third Wheel, Diary of a Wimpy Kid: Hard Luck, Diary of a Wimpy Kid: The Long Haul, Diary of a Wimpy Kid: Old School, Diary of a Wimpy Kid: Double Down na Diary of a Wimpy Kid: The Gateway

“Hii ni orodha ya kwanza, baada ya kuhakiki na kuthibitisha kuwa vitabu hivi vinakiuka mila na desturi, yaliyomo ndani yake si mazuri kwa malezi ya  watoto wa kitanzania, uhakiki unaendelea,” alisema Prof Mkenda.

Aidha aliwataka wazazi kuangalia mara kwa mara mifuko ya watoto wao ili kuhakikisha hawatumii vitabu hivyo maana vinahatarisha ubora wa elimu kwa watoto.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags