Selena Gomez achumbiwa na Blanco

Selena Gomez achumbiwa na Blanco

Picha za mwanamuziki na mwigizaji wa Marekani Selena Gomez zimezua maswali kwa mashabiki wakiuliza kama msanii huyo amechumbiwa na mpenzi wake Benny Blanco.

Maswali hayo yamekuja baada ya Gomez kuchapisha picha akiwa na mpenzi wake huyo huku akifunika kidole chake cha peta na emoji ya kopa.

Mbali na kuficha kidole hicho mkali huyo wa ‘Only Murders in the Building’ ameoneakana akifuatilia akaunti ya ‘CMG Weddings & Events’ mara kwa mara inayojihusisha na masuala ya uandaaji wa sherehe mbalimbali nchini Marekani.

Ikumbukwe kuwa Selena Gomez alithibitisha kuwa kwenye mahusiano na Benny Blanco Desemba 2023 kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika kuwa Blanco ndiye kila kitu kwenye maisha yake yaliyobaki.

Mbali ya kuwa kwenye penzi zito wawili hao pia wamewahi kutoa ngoma ya pamoja iitwayo ‘I Can’t Get Enough’ iliyotoka mwaka 2021.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags