Mwanamuziki wa Marekani Selena Gomez na Mpenzi wake Benny Blanco wametangaza kuchumbiana baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Selena Gomezi mwenye umri wa miaka 32 amewaka wazi uchumba huo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuchapisha picha ikimuonesha amevaa pete ya uchumba ikisindikizwa na maneno "Forever Begins now".
Gomez na mchumba wake Benny Blanco mwenye umri wa miaka 36, wameshirikiana kwenye kazi kadhaa za Muziki ikiwemo "Same Old Love" iliyotoka 2025 kabla ya kuingia kwenye mahusiano 2023 baada Gomezi kuweka wazi mahusiano hayo Desemba 2023.
"Yeye ni kila kitu kwangu kabisa moyoni mwangu amekuwa jambo bora zaidi ambalo limewahi kunitokea bado ni bora kuliko mtu yeyote ambaye nimekuwa naye Ukweli,” aliandika Gomez.
Leave a Reply