Sean Kingston asimamishwa kizimbani

Sean Kingston asimamishwa kizimbani

Mwanamuziki wa Marekani Sean Kingston siku ya jana Juni 4,2024 alisimamishwa kizimbani kutokana na tuhuma zinazomkabili za kuiba vitu vyenye thamani ya dola 1 milioni ikiwa ni sawa na Sh 2.6 bilioni.

Video zilizosambaa katika mitandao ya kijamii zilimuonesha akiwa katika mahakama ya jimbo la Broward, Florida Nchini humo. Ikumbukwe Kingston na mama yake walifunguliwa mashitaka wakituhumiwa kwa wizi.

‘Rapa’ huyo alikamatwa siku chache baada ya kushitakiwa huku mama yake mzazi Jernice Turner (61), akitiwa nguvuni na polisi Mei 23 mwaka huu nyumbani kwa mwanaye huko Southwest Florida.

Kwa mujibu wa maelezo ya waendesha mashitaka walieleza kuwa Kingston na mama yake wanatuhumiwa kuiba vitu mbalimbali vyenye thamani Sh 2.6 bilioni ambavyo ni Vito vya thamani, fedha kutoka kwenye kampuni ya Escalade na benki ya ‘Bank Of America’.

Pia wanadaiwa kufanya wizi katika benki ya First Republic Bank pamoja na kumuibia mtu wa Furniture.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags