Saraphina: Sina tatizo na Ruby sijui yeye

Saraphina: Sina Tatizo Na Ruby Sijui Yeye

Msanii Saraphina anayetamba na ngoma yake  'Upo nyonyo' Amenyoosha Maelezo kuhusu ukaribu wake kwa sasa na msanii mwenzie ruby baada ya kuwepo maneno ya chinichini kuwa wawii hao hawana mahusiano mazuri mara baada ya kufanya wimbo pamoja.

Baada ya tetesi hizo za chini chini Msanii Saraphina ameamua kulijibia suala hilo na kuweka wazi masuala hayo.

''Tupo fiti lakini sijui yeye, mimi sijawahi kuwa karibu sana na Ruby hata kuanzia mwanzoni tulikua tu marafiki wasanii tunasapotiana lakini vile vile yeye alikuwa anawasiliana sana na meneja wangu, “

“So tulikutana studio kabla ya kufanya wimbo na ndio ilikuwa mara ya kwanza tunakutana na tukasalimiana na kisha akaniambia tufanye kazi pamoja tukaingia studio tukafanya na wimbo ukawa mzuri tukashoot na video wimbo ukawa mkubwa na watu wakaupenda tulivyokuwa tunaongea zamani na sasa ni vilevile haijabadilika'' Saraphina.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post