Sancho ndiyo basi tena Man United

Sancho ndiyo basi tena Man United

‘Kocha’ wa Manchester United Erik ten Hag ameweka wazi kuwa hakuna njia ya kurudi kwa #JadonSancho katika ‘klabu’ hiyo baada ya kushinikiza mshambuliaji huyo kuuzwa mwezi Januari.

Sancho hakuweza kucheza katika ‘timu’ hiyo tangu ushindi wa 3-2 dhidi ya Nottingham Forest mwishoni mwa Agosti baada ya kupinga kauli ya ‘kocha’ huyo akiwa mazoezini.

Uamuzi wa kumhamisha Sancho ulifikiwa baada ya nyota huyo wa zamani wa Borussia Dortmund kukataa kuomba msamaha kwa Ten Hag kufuatia mazungumzo ya mgogoro na ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo.

Inadaiwa kuwa ‘Klabu’ ya #JuventusFC inaangalia uwezekano wa kumpata mchezaji huyo kwa mwezi Januari.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags