Sancho afuta account yake ya Instagram

Sancho afuta account yake ya Instagram

Mchezaji wa ‘klabu’ ya Manchester United Jadon Sancho awashangaza mashabiki wake baada ya ukurasa wake wa Instagram kutoonekana tena huku wengine wakidai kuwa huenda mchezaji huyo amefuta account hiyo au amehama 'timu' kutokana na ugomvi wake na ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo Erik ten Hag.

Ikumbukwe kuwa 'winga' huyo aliondolewa kwenye kikosi cha Man United baada ya kutofautiana na ‘kocha’ wa ‘timu’ hiyo pindi alipomshutumu ‘kocha’ huyo kueneza habari za uongo.

Licha ya  wachezaji wenzake katika ‘klabu’ hiyo akiwemo Harry Maguire, Luke Shaw na Marcus Rashford, wamejaribu kumshauri Sancho aombe msamaha ili kurejea kikosini, huku Chama cha Wanasoka wa Kulipwa kikimsaidia 'winga' huyo kupata suluhu.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags