Salha afunguka, Sababu muziki wa taarab kusuasua

Salha afunguka, Sababu muziki wa taarab kusuasua

Mwanamuziki wa taarab, Salha Abdallah, ametoa ufafanuzi juu ya changamoto zinazokumba muziki wa taarabu na jinsi ambavyo umepoteza umaarufu wake katika miaka ya hivi karibuni.

Salha, ambaye pia amejikita katika uigizaji, ameeleza kuwa muziki wa taarab umekuwa ukikabiliwa na mabadiliko makubwa, na sasa unapoteza mwelekeo wake wa asili.

“Wasanii wengi wa taarabu hawataki kujishughulisha wao wenye katika kupambania muziki wao hivyo wamekuwa tegemezi, kila kitu wamewaachia viongozi wanaowasimamia au wa Band ndiyo maana sasa hivi wanaosikika ni wachache mfano utamsikia Aisha Vuvuzera, Rahma Machupa labda na mimi basi” amesema

Aidha, Salha alizungumzia suala la malipo duni kwa wasanii wa taarabu na jinsi linavyochangia kushuka kwa ubora wa muziki.

“Kingine wasanii wa taarab hawalipwi vizuri hata wakiandaa show, kwa sabab unaweza kukuta pesa ambayo anatakiwa kulipwa msanii mmoja katika show wanalipwa wasanii kumi wa taarabu hiyo inapelekea hata ukimwalika mwimbaji taarabu kwenda kutumbuiza akifika eneo la tukio kachoka,”amesema.

Aidha Salha amegusia baadhi ya band za Muziki wa taarab wamekuwa wakirudia rudia nyimbo ambazo zilifanywa na wakonge wa taarabu kama akina Sabaha Salum, Mwanahawa Ally.

“ Sasa hivi hakuna jipya kwenye hizi band zetu za taarab nyimbo zimekuwa zikijirudia yaani wasanii wa sasa hawana nyimbo za taarabu kabisa na wamehamia kwenye TaaraDance na siyo taarab hasilia hivyo unakuta hata kwenye masherhe wasichana wa sasa hivi wanaamua kucheza nyimbo za zamani maana ndiyo nzuri” amesema.

Mbali na hayo Salha ametoa rai kwa viongozi wa band za taarabu na wasanii wa muziki huo wabadilike kutokana na wakati.

“ Hivyo basi taarabu ibadilike hasa kwa viongozi na wasanii wenyewe tupo wakati wa kidijitali mfano sasa unaweza kukuta msanii wa taarab hatumii hata Instagram, wala Tiktok utakuta yupo Facebook huko na anaishi ku-post vijembe tu visivyo na maana” amesema Salha.

Utakumbuka kuwa Salha amewahi kufanya nyimbo kama Chozi langu utalilipa, Nanisumbua, Kuolewa, Ubinafsi na Uchoyo, na nyingine nyingi ambapo hivi karibuni ameingia katika masuala ya ugizaji akionekana katika tamthilia ya Kombolela na Siri.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post