Sakata la Ruby kutamani kufa, Meneja wake afunguka

Sakata la Ruby kutamani kufa, Meneja wake afunguka

 

Moja kati ya stori ambayo imezua gumzo mitandaoni ni hii hapa inayomuhusu msanii wa muziki wa bongo fleva Ruby ambaye alishare taarifa kupitia account yake ya instagram ambapo ujumbe huo alioandika uliibua maswali mengi kwa mashabiki zake.

Ruby aliandika kupitia IG yake kuwa anatamani kufa ili apumzike na mambo ya dunia.

Sasa bwana taarifa kutoka kwa Meneja wa msanii huyo Andrea Wayayu ameeleza sababu za Ruby kuandika ujumbe huo mtandaoni.

“Maisha binafsi ya Ruby na changamoto za kibinaadam ndio zimetokea mpaka kuandika anatamani kufa ili apumzikie na dunia.”

Meneja wake ameongeza kusema kuwa  kuna muda mtu unapitia magumu, kushikilia mambo mengi moyoni na kukosa nafasi ya kuongea na mtu au watu na kuhisi duniani sio sehemu sahihi ya kuishi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags