Safari ya Dj Mamie katika tasnia yake

Safari ya Dj Mamie katika tasnia yake

Mamboz guys!! Hivi unajua hii ni weekend nyengine mwamba ni kawaida yetu lazima tukuwekee kitu kizuri katika michezo na burudani ili usikae kinyonge mtu wangu wa nguvu.

Leo katika Burudani tunakusogezea ladha tofauti mwanetu tunataka ujue umahiri wa Dj Mamie kwenye majukwaa mbalimbali anavyo kiinukisha mtoto wakike.

Kwanza kabisa kabla sjakupeleka kwenye point naomba nikujuze kitu kwamba sikuhizi mambo yamekuwa tofauti tulikuwa tukiwaona ma Djs wakiume pekee lakini siku hizi mwamba mambo yameenda kasi wanawake wamekuwa kipaumbe na wanakinukisha sana kwenye talanta hiyo.

Mariamu Lugiko Lushinda maarufu kama DJ Mamie bila shaka ndie mkubwa zaidi kwa hapa Tanzania katika kizazi kipya cha wanawake ma Djs akiwa na umri mdogo wa miaka 27.

Ni moja kati ya DJs walio wahi kupata tuzo za mashindano ya muziki wa Tanzania mwaka huu april 29 kwenye Super dome.

Ebana! Mwanetu mimi sijui mengi kuhusu kubadili, kuchanganya, na kunakili nyimbo lakini unapohudhuria moja ya vibe lake unaweza kusema kuwa yeye ni gwiji kwenye industry DJs.

Hii imechangia kwa kiasi kikubwa Dj Mamie kukubalika kwenye vipindi vya redio, televisheni juu ya aina tofauti za kubadilisha Afrobeats, RnB, Amapiano, na nyengine nyingi.

Hivyo basi Mwananchi Scoop tulimpa wasaa wa kuelezea ni kwa namna gani anafaulu katika kazi yake.

“Niko vizuri kwasababu huwa napata habari za sasa muziki ambao mimi hutafuta kutoka kwa vidimbwi (sehemu za kula bata), rekodini,  mtandaoni, tovuti za muziki, tovuti za mitandao ya kijamii, podikasti, blogu na hata kusikiliza kwa DJs wengine,” alisema Dj Mamie.

Aliongeza kuwa “mimi siku zote napenda kujishugulisha na hadhira (audience) zaidi kwa kuwauliza maswali ni nyimbo gani zinasikilizwa sana”

Lakini alizidi kutueleza ndoto yake ya kuwa Dj ilikuwa ndani ya damu hivyo alikuwa akiifatilia talanta yake taratibu hadi alipo hitimu shahada yake ya kwanza katika upande wa sayansi siasa na umma katika chuo kikuu cha Dar es salaam.

Ndipo alipo chukua maamuzi ya kuwa serious baada ya kukutana na Dj AllyB alipo kuwa Dj huko Maisha Club anasema.

“Wakati huo nilipokutana naye, nilivutiwa sana alivyo kuwa akifanya Dj AllyB baadaye alitangaza chuo chake cha Dj nilimfuatilia ili kupata nafasi na kutoka hapo kila kitu kilianza kwenda kama nilivyotamani zamani” alieleza Mamie

Jambo hilo lilichangia familia yake kutoka Mwanza kuja Dar kwaajili yake “Nakumbuka siku moja baba angu aliniona kwa Tv alishangaa kwa sababu hawakujua nini nafanya tokea nilivyo kuja Dar baada ya masomo yangu alifurahi sana kuniona”alisema Mamie.

Anafurahi kuwa baba ake ndio mfuasi wake mkuu akimsapport kwa kile anacho kifanya.

 SAFARI YAKE KATIKA U DJ

Safari yake katika talanta yake mwanadada huyo alianza kuwaburudisha watu kutoka kwenye matamasha mbalimbali mjini moja kati ya tamasha kubwa aliloanza kufanya la Soggy Doggy.

Hapo ndio ukawa mwanzo wakupata madili tofauti tofauti kwenye media kama EFM.

Mnamo 2020, alipata kazi yake ya kwanza katika kituo cha redio cha EFM ambapo alipata nafasi ya kucheza muda wote katika vipindi vya redio kwa kawaida aliwafanya watu waruke naye na list yake ya kucheza miziki isio tabirika yenye nguvu ya kustaajabisha na kupunga mkono hewani kwa vibe.

Baadaye alihamia Wasafi FM baada ya Mkurugenzi Mtendaji wa WCB Diamond Platnumz kushare video zake kwenye akaunti yake ya Instagram wakati akitumbuiza.

“Nilimwomba Romy Jons anipe nafasi kwenye tamasha nifanye free na akakubali kuniunganisha na wenyeji, basi huku mimi nilikuwa nafanya kipindi changu Diamond alikuwa anatazama TV na alirekodi kipande changu na kuweka kwenye instastor yake,” anaeleza Mamie.

Kupitia hilo aliweza kuongeza umaarufu zaidi na kuonekana katika matamasha kubwa ya nchi.

Matamasha hayo ni pamoja na matamasha ya Mziki Mnene, Wasafi Festivals, Kongo Goma Amani Festival, Rwanda pamoja na Lady Jaydee, na tamasha la Comoro na Zuchu.

Orodha zake kubwa za kucheza, chaguo la muziki na mpangilio, vibe, na mtindo wa hyping umefanya mashabiki kuomba vikao zaidi kama alicheza kwenye vituo vya redio au kwenye matamasha.

Licha ya hayo Mamie anaamini kwamba, kutambuliwa kama mtaalamu na kuheshimiwa kinachohitajika ni ubunifu, mdundo, na ujuzi wa kiufundi.

“Kuwa hapa nilipo leo sio rahisi, unahitaji kuelewa muundo wa muziki, kuwa na uwezo wa kufanya katika kila aina ya hali, jua vifaa vyako vya Dj, shirikiana na aina tofauti za watu, na uweze kujitangaza kama DJ,” anaeleza.

Kwa mantiki hiyo basi nikwambie mwanetu hakuna haja ya kusema hakuna fursa ya kufanya talanta yako kikubwa ni kufanya kazi watu waone utofauti wako na watu wengine mwamba sio walalamika tu take action ona mambo yanavyoenda yenyewe.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags