Sababu za kutokwa machozi wakati wa kukata kitunguu

Sababu za kutokwa machozi wakati wa kukata kitunguu

Kuna kitendawili kisemacho nampiga mwanangu nalia mwenyewe, jibu lake kitungu, kitendawili hiki kimetokana na tabia ya tunda hilo ambalo wakati wa kulikata hupelekea mkataji kutoka machozi.

Wengi wanaamini kuwa machozi hayo hutokana na majimaji yaliyopo kwenye kitunguu bila ya kufahamu nini hasa husababisha macho kuwasha na kutokwa machozi tofauti na ilivyo kwenye nyanya.

Kwa mujibu wa wanasayansi wanaeleza kwamba machozi hutoka wakati wa kukata kitunguu kwa sababu ya kemikali inayoitwa syn-propanethial-S-oxide ambayo husisimua tezi ya macho iitwayo lachrymal ambayo kazi yake ni kuzalishaji machozi.

Inaelezwa kuwa wakati unapokata kitunguu, kisu kinavunja seli za kitunguu na kusababisha kemikali hiyo kutoka nje, hivyo basi inapokutana na majimaji ya jicho hubadilika na kuwa asidi ya sulfuric ambayo huathiri neva zilizo karibu na macho, na mwili unaona kama ni kitisho hivyo hutoa machozi ili kujaribu kusafisha kemikali hiyo na kumlinda mtu kutokana na madhara zaidi.

Hivyo kuvaa miwani wakati wa kukata kitunguu au kuweka kitunguu kwenye maji baridi kabla ya kukata kunaweza kupunguza athari za machozi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags