Sababu Serikali ya Ethiopia, Saudi Arabia kutotumia red carpet

Sababu Serikali ya Ethiopia, Saudi Arabia kutotumia red carpet

Nchi nyingi zimekuwa na sifa mbalimbalia ambazo hutumika kama kielelezo chake, ukitaka kufahamu historia ya  Ethiopia lazima ugusiwe kutotawaliwa kwake, na kuhusu Saudi Arabia lazima uelezwe kuhusu maua yenye rangi ya zambarau yaotayo jangwani.

Kuachana na kutotawaliwa kwa Ethiopia na maua yaliyopo Saudi Arabia, pia kumekuwa na sifa nyingine ya kipekee katika nchi hizo, za kutotumia zulia jekundu (red carpet), badala yake Ethiopia hutumia zulia la rangi ya kijani na maua ya njano, Saudi Arabia hutumia la zambarau.

Mazulia hayo nyenye rangi hizo hutumika katika matukio maalumu ya kitaifa, yakiwa na maana kubwa, Saudi Arabia hutumia rangi hiyo kuwakilisha maua ya asili yaliyopo jangwa la Saudi Arabia.

Ethiopia ni tofauti, huamini matumizi ya zulia la kijani ni sehemu ya sera ya maendeleo endelevu, matumizi ya teknolojia ya kisasa, kukuza historia, utamaduni, maadili na urithi wa Ethiopia. Zulia hilo hutengenezwa na kampuni ya Ethiopia, ‘Aklill Company’, wanaliita Adey Abeba Carpet.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags