Katika mahojinao yake na ‘Armchair Expert ya Dax Shephard’ Chopra ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 43 ameeleza kuwa alichukua uamuzi huo kwa lengo la kutimiza ndoto zake.
“Nilihifadhi mayai yangu ya uzazi nikiwa na miaka 30, ilinipa uhuru kuendelea na njia yangu ya kufikia malengo makubwa niliyotaka. Nilihitaji kufika mahali fulani katika kazi yangu. Pia, sikuwa nimekutana na mtu niliyependa kupata naye watoto au sikuwa naona hilo likitokea.
“Hilo lilikua linanipa wasiwasi. Nilipofikisha miaka 35, mama yangu ambaye ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi akaniambia, ‘Ukifikisha 36 fanya tu,” amesema Chopra

Hata hivyo alitoa ushauri kwa mabinti wadogo kuhifadhi mayai yao kwakuwa kuna asilimia ndogo ya kupata mtoto ukiwa na umri wa miaka 35.
“Nawaambia rafiki zangu wote wa kike walioko katika umri mdogo kuwa saa ya kibaolojia ni ya kweli kabisa. Inakuwa ngumu sana kupata mimba baada ya miaka 35 na kuibeba hadi ukamilifu wa muda wa kujifungua na mambo yote hayo, hasa kwa wanawake ambao wamekuwa wakifanya kazi maisha yao yote.
“Lakini sayansi ipo katika hatua ya kushangaza sana kwa sasa. Hii ni zawadi bora kabisa utakayojipa mwenyewe kwa sababu unachukua nguvu kutoka kwa saa yako ya kibaolojia, na unaweza kuendelea kufanya kazi kwa muda wowote unaotaka. Mayai yako yataendelea kuwa na umri uleule uliyoyahifadhi,”amesema
Hata hivyo mwigizaji huyo ameongezea kuwa wakati anafunga ndoa na mwanamuziki Nick Jonas mwaka 2018 alitamani sana kupata mtoto lakini changamoto kubwa ilikuwa mume wake huyo kama angetamani kuwa baba akiwa na umri wa miaka 25.
Aidha baada ya kukubaliana Chopra alitamani kupata mtoto kwa njia ya kujamiiana lakini ilishindikana ndipo wawili hao walikodisha tumbo la mwanamke mwingine kwa ajili ya kubeba mimba kupitia mayai ya Chopra yaliyohifadhiwa. Ambayo yalirutubishwa kwa mbegu za Nick ndipo wakafanikiwa kupata mtoto wao kwa kike aitwaye Malti Marie aliyezaliwa mwaka 2022.
Chopra amefahamika kupitia filamu alizozifanya ikiwemo Heads of State, Quantico, Baywatch, Krrish, Bajirao Mastani, The Matrix Resurrections, Barsaat, Teri Meri Kahaani na nyinginezo huku mumewe akionekana katika filamu kama Jumanji: Welcome to the Jungle, Camp Rock na Careful What You Wish For.
Mbali na Chopra mastaa wengine ambao wamehifadhi/kugandisha mayai yao ya uzazi ni Kourtney Kardashian, mwigizaji Olivia Munn, Halsey, Rita Ora, Paris Hilton, Mwigizaji wa ‘Modern Family’ Sofia Vergara na wengineo.
Kuhifadhi au kugandisha mayai ‘Egg Freezing’ ni nini ?
Kuhifadhi mayai (Egg Freezing) ni mchakato wa kitabibu ambapo mayai ya uzazi ya mwanamke hukusanywa kutoka kwenye ovari, kisha hugandishwa (kwa kutumia teknolojia ya vitrification) na kuhifadhiwa kwa muda mrefu ili yatumike baadaye kupata ujauzito.
Ni njia inayotumiwa hasa na wanawake wanaotaka kuchelewesha kupata watoto kwa sababu za kiafya, kielimu, au kazi, au kwa sababu bado hawajapata mwenza wa maisha. Inasaidia kuhifadhi uwezo wa kupata mtoto hata baada ya umri kuendelea.
Leave a Reply