Ruger: Naacha Muziki

Ruger: Naacha Muziki

Mwanamuziki kutoka Nigeria Ruger amedai kuwa anataka kuacha muziki ili aweze kuwa video king, hii ni baada ya kuonekana kwenye video ya wimbo kutoka katika kundi la Clean Bandit.

Katika ukurasa wake wa Instagram Ruger amechapisha kipande cha video akionekana kama video king katika wimbo uitwao ‘Cry Babby’ wa kundi hilo na kudai kuwa anaona video king inamfaa zaidi kuliko kuimba.

“I’m leaving music to become a video vixen 🙏🏾 CRY BABY” akiwa na maana kuwa anaacha muziki ili kuwa video vixen.

Clean Bandit ni kikundi cha muziki cha kutoka Uingereza, kundi hilo lililoundwa huko Cambridge mwaka 2008 linawashiriki watatu wawili wakiwa wanaume na mmoja akiwa mwanamke, wamekuwa wakitamba na vibao vyao kama ‘Solo’, ‘Rockabye’, ‘Baby’ na nyinginezo.

Kwa upande wa Ruger amekuwa akitikisa Nigeria na nchi jirani kupitia nyimbo zake kama ‘Girlfriend’, ‘Make Way’, ‘Asiwaju’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags