Ruger afunguka sababu za kuondoka Jonzing World

Ruger afunguka sababu za kuondoka Jonzing World

Mwanamuziki kutoka nchini Nigeria Ruger amefunguka mazito kuhusiana na sababu iliyomfanya atemane na lebo yake ya zamani iitwayo ‘Jonzing World’ kwa kudai kuwa walikuwa wakimnyonya.

Ruger kupitia ukurasa wake wa X ameweka wazi kuwa alikuwa hatendewi haki katika lebo hiyo kwani walikuwa wakitumia pesa zake kumfadhili msanii wao mpya huku yeye wakimuacha gizani.

Hata hivyo ameeleza kuwa anaithamini sana lebo hiyo kwakua ilimtambulisha kwenye game lakini ilishindwa kumpush kimuziki ili aweze kukua zaidi.

Ruger alisaini mkataba na ‘Jonzing World’, mwaka 2021 na kuondoka kwenye lebo hiyo mwanzoni mwa mwaka huu ambapo kwasasa anafanya kazi na lebo yake ya ‘Blown Boy Entertainment’.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags