Ruby amtupia dongo Kusah

Ruby amtupia dongo Kusah

Aloooooh! Mambo ni mengi, muda ni mchache. Mapenzi jamani haya mmmh! Basi moja ya story kubwa inayotembea sana kwenye mtandao wa kijamii inamuhusu msanii wa bongofleva Ruby  kumtolea dongo mzazi mwenzie, kusah.

Ikumbukwe wawili hao waliwahi kuwa na mahusiano na kujaliwa mtoto mmoja. Katika mahojiano na kituo maarufu cha habari, mwanadada huyo alifunguka kuhusiana na mahusiano yake mapya na kujibu swali la mashabiki zake kwa kumfananisha kimo na muonekano Kusah na mpenzi wake mpya.

Msanii amejibu swali hilo kwa kusema, "Mpenzi wangu wa sasa yuko tofauti sana hata kimuonekano kwani mpenzi wake wa aasa kichwani ana rangi nyeusi na yule wa zamani ana ubuyu kichwani."

"Niwaambie tu kuwa mpenzi wangu wa sasa hivi kichwani rangi yake ni nyeusi lakini mpenzi wangu wa zamani kichwani ana ubuyu," alisema Ruby.

Aiseeeee! Nyie nyie, unaambiwa mitandao ya kijamii imefurika kwa mapovu ya waja wakisema kuwa mwanadada huyo bado anamtaka ex wake. Je wewe mwanangu sana unahoja? Dondosha comment yako hapo chini.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post