Roy Keane apigwa na shabiki wa Arsenal

Roy Keane apigwa na shabiki wa Arsenal

Baada ya Manchester United kupoteza mchezo kwa mabao 3-1 dhidi ya Arsenal mchambuzi wa ‘timu’ hiyo, Roy Keane anadaiwa kupigwa kichwa na shabiki wa Arsenal, huku mchezaji wa zamani wa Manchester City, Micah Richards akiwatenganisha wawili hao.

Aidha tukio hilo linadaiwa kutokea wakati Keane akielekea kutekeleza majukumu yake ya uchambuzi baada ya ‘mechi’, huku, Jarida la Daily Mail likidai kwamba Keane alivamiwa na shabiki mmoja wakati akisubiri lifti, shabiki aliyempiga kichwa kilichoishia kumgusa kifuani na kidevuni.

Licha ya walinzi kuingilia kati huku Michah Richards akionekana kumshikilia mtu huyo shingoni, kabla ya mtu huyo kuondolewa mpaka sasa haijajulikana chanzo cha kupigwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags