Rosa Ree awajibu mashabiki zake

Rosa Ree awajibu mashabiki zake

Rapper kutoka nchini Tanzania Rosary Rober maarufu kama Rosa ree ametoa povu kwa Kuwajibu Baadhi Ya Mashabiki Wake Ambao Walikua Wakidauti Kuvalishwa Kwake Pete Kuwa Huenda Ikawa Mapema Sana Kwa Kile Wanachoamini Kuwa Kutasababisha Aache Kuutumikia Muziki Wa Bongo Fleva.


Rosa Ree amefunguka hayo wakati akiwa katika mahojiano na chombo cha habari kilichop nchini na kueleza kuwa ‘’Sasa hivi Mimi ni mchumba wa mtu na nimefurahi Sana Kwasababu nimetoka nae mbali sana, Tumepanga Mengi Sana na Tunaomba Mungu atusaidie Tufanikishe''
Aliendelea kwa kueleza "Wapo ambao watasema mimi bado ni mdogo? lakini mimi naamini kwamba pale unapokuwa na nguvu ndio muda mzuri na Kupanga Future Yako, Kwenye Majukumu ya Muziki naamini muziki upo na utaendelea Kuwepo napenda muziki tangu nikiwa mdogo hadi sasa hivyo hata nikiwa mzee nitaendelea kuupenda'' amesema Rosa Ree


Hata hivyo alimalizia kwa kusema "Ukisema muziki ufanye nisifanye maisha mengine haitakua sawa, kwaiyo ukisema nikifika miaka 50 ndio nianze kutafuta mwenza itakua Uongo , kifupi watu waendelee kusapoti muziki wangu wajue pia sitawaangusha (Kwenye Muziki) na naamini kuna kitu wanaweza kujifunza kwenye maisha yangu'' amesema.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags