Ron afariki akiwa na miaka 66

Ron afariki akiwa na miaka 66

Muigizaji mkongwe kutoka Marekani, Ron Cephas Jones amefariki siku ya jana akiwa na umri wa miaka 66, imeripotiwa kuwa muigizaji huyo amefariki kutokana ugonjwa wa mapafu uliomsumbua kwa muda mrefu licha ya mwaka 2020 alitakiwa kupandikizwa mapafu.

Kwa mujibu wa TMZ inaelezwa kuwa baada ya kifo chake baadhi ya waigizaji waliungana mtandaoni kushiriki na kuomboleza taarifa za nyota huyo.

Mbali na movie yake ya “This Is Us,"  Cephas aliigiza katika vipindi vingine vya televisheni vikiwemo “Law & Order: Organised Crime", “Better Things,” “Luke Cage” na “Looking For Alaska”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags