Roberto Oliveira aenda Brazil

Roberto Oliveira aenda Brazil

 

Taarifa kutoka klub ya Simba imeleezwa kuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo Roberto Oliveira ameondoka Usiku wa kuamkia leo (Januari 24) kwenda kwao Brazil kwa shughuli binafsi za Kifamilia.

Aidha Kocha huyo anatarajiwa kurejea mwishoni mwa Mwezi huu wa Januari.

Roberto mwenye umri wa miaka  (62) ameondoka akiwa na Siku 21 tuu toka ajiunge na Wekundu wa Msimbazi akitokea Vipers ya Uganda baada ya kutambulishwa rasmi Januari 3, 2023.

Hata hivyo Kocha huyo alijizolea umaarufu Afrika Mashariki kutokana na kuisuka vizuri Vipers SC ya Uganda ambao ndio waliwatoa TP Mazembe kwenye Club Bingwa Afrika msimu huu.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post