Rihanna bado hana mpango wa kufanya ziara

Rihanna bado hana mpango wa kufanya ziara

Baada ya kuzuka tetesi kuhusiana na msanii #Rihanna kuwa anapanga kufanya #Tour kubwa mwaka 2024, kwa mujibu wa #Billboard imefichua taarifa hizo ni za uongo.

Siku ya Jumapili baadhi ya vyombo vya habari nchini #Marekani viliripoti kuwa #Rihanna anatarajia kufanya ziara kubwa Dunia ambapo ameingia mkataba wa Dola 39 milioni na Live Nation.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu cha msanii huyo kimeeleza kuwa Rihanna bado hajathibitisha ziara yoyote kwa mwaka 2024.

 Aidha Billboard inaripoti kuwa Live Nation haijafika kwenye kumbi zozote kufanya booking kwa ajili ya ziara yoyote.

Ikumbukwe ziara ya mwisho aliyoifanya ni mwaka 2016 ya ‘Anti World Tour’ ambayo aliingiza zaidi ya dola 100 milioni kwa mauzo duniani kote huku sehemu ya mwisho ya zaira hiyo ikiwa ni ‘Abu Dhabi’ Novemba 27, 2016 na mpaka sasa hajafanya tena ziara yoyote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags