Rihanna afunguka kuhusu ujauzito na kustaafu muziki

Rihanna afunguka kuhusu ujauzito na kustaafu muziki

Baada ya kuzuka tetesi kupitia mitandao ya kijamii kuhusiana na mwanamuziki kutoka visiwa vya Barbados, Rihanna kutarajia kupata mtoto wa tatu na mpenzi wake A$AP Rocky, msanii huyo amekanusha uvumi huo.

Riri ameyasema hayo wakati alipokuwa kwenye uzinduzi wa nywele za ‘Fenty Hair’ ambapo aliiambia ‘Entertainment Tonight’ kuwa kwa sasa hana ujauzito lakini yupo tayari kupanua familia kwa siku za mbeleni.

Hata hivyo mkali huyo wa ngoma ya ‘Diamonds’ alifunguka kuhusaina na ‘tisheti’ yake iliyoandikwa nimestaafu kwa kuweka wazi kuwa hana mpango wa kustaafu kuimba muziki lakini anajipanga kurekodi ngoma mpya.

“Muziki kwangu ni uvumbuzi mpya ninagundua vitu tena, nipo tayari kurudi studio, ninaanza upya, lakini sitaki kupuuza nyimbo nilizo nazo.

“Kwa hivyo nataka kurudi nyuma na kusikiliza vitu kwa masikio mapya na mtazamo wangu mpya na kuona kinachotumika na kile ambacho bado ninakipenda” alisema.

Ikumbukwe kuwa siku tatu zilizopita Riri alikatisha mitaa ya New York akiwa amevalia ‘tisheti’ iliyoandikwa ‘I AM RETIRED’ ikiwa na maana amestaafu jambo ambalo limewakatisha tamaa mashabiki wengi kusubiri albumu mpya kutoka kwa mwanamuziki huyo huku mara ya mwisho kuachia album ikiwa ni Januari 2016 iitwayo ‘Anti’.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags