Rick Ross aweka mpunga mrefu, kurekebisha mjengo wake

Rick Ross aweka mpunga mrefu, kurekebisha mjengo wake

Baada ya kununua jumba la kifahari kwa dola 35 milioni kwenye kisiwa cha Star kilichopo Miami nchini Marekani mwaka 2023, ‘rapa’ Rick Ross ameripotiwa kufanya marekebisho ya jumba hilo kwa kupanua mjengo huo futi za mraba 4,000.

Imeelezwa kuwa Rick amewekeza kiasi cha dola 20 milioni kwa ajiri ya marekebisho ambapo ukarabati huo utajumuisha Bwawa la Samaki adimu la Kijapani ‘Koi’ Studio kubwa ya kurekodia pamoja na bwawa la kuogelea.

Licha ya msanii huyo kuendelea kuonesha jeuri ya fedha, mwezi Januari pia aliweka wazi kuwa anampango wa kujenga nyumba chini ya Ardhi ambayo itakuwa na chumba cha kulala, gereji na mashine inayotengeneza maji kutoka angani.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags