Rick Ross atakiwa kulipia ada ya mtoto zaidi ya sh 500 milioni

Rick Ross atakiwa kulipia ada ya mtoto zaidi ya sh 500 milioni

Moja ya stori inayoendelea kusambaa kupitia mitandao ya kijamii ni kuhusiana na aliyekuwa mpenzi wa ‘rapa’ Rick Ross aitwaye Tia Kemp kutaka kiasi kikubwa cha pesa cha ada ya mtoto wao mkubwa aitwaye William Roberts III.

Kufuatia na video inayoendelea kusambaa katika mitandao ya kijamii inamuonesha mpenzi wa zamani wa Rozay akimtaka mtoto wake ampigie simu baba yake aweze kumtumia kiasi cha dola 200K sawa na Sh 540 ya ada ya masomo ya chuo kikuu.

“Sifanya mchezo hapa, nataka umpigie baba yako na umtumie screenshot hicho kinachoonekana hapo kisha umwambie hicho ndicho ninachohitaji kwenye akaunti yangu ya benki na nataka anitumie sasa hivi nahitaji robo ya dola milioni 1” amesema mzazi mwenzie wa Rick Ross

Hata hivyo ukiachilia mbali kulipa pesa hizo, siku chache zilizopita Rick alitoka kusheherekea kumlipa mzazi mwenzie huyo pesa za matunzo ya mtoto wake huku cha ajabu kilichonacho wavuruga watu ni kudai tena kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya ada.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags