Rick Ross ajitolea kumsaidia Kanye West

Rick Ross ajitolea kumsaidia Kanye West

‘Rapa’ kutoka nchini Marekani #RickRoss amejitolea kutaka kumsaidia Kanye West kuisambaza albumu yake mpya kwa kutumia label yake ‘Maybach Music Group’ (MMG), baada ya mwanamuziki huyo kukosa usaidizi wa kuisambaza albumu yake mpya.

‘Wiki’ iliyopita iliripotiwa kuwa Kanye alipanga kuachia albumu yake mpya Oktoba 13, 2023, ambayo inatajwa kuwa na ngoma za Kanye West za takribani miaka mitano iliyopita.

Lakini wasambazaji wengi wamekuwa wakiikwepa kutokana na kauli tata za msanii huyo dhidi ya Wayahudi alizozitoa mwaka 2022.

Ikumbukwe kuwa albamu ya mwisho kutoka kwa Kanye West ni #DONDA2 ilitoka Februari 23, 2022 kwa utaratibu wa kuuzwa kupitia kifaa cha muziki cha ‘#StemPlayer.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags