Rich mitindo: dunia ninayoishi ni zaidi ya pepo

Rich mitindo: dunia ninayoishi ni zaidi ya pepo

Wakiwa katika kufurahia kumbukizi ya siku ya kuzaliwa mtoto wao #Richmitindo amempa pongezi mke wake #JacklineWolper, kwa kuwa mama bora na mke bora kwake siku zote ambazo wapo pamoja.

Rich amemwagia sifa mama watoto wake, kupitia ukurasa wake wa #Instagram kwa kuandika,

“Kila nikiangalia hii picha sina cha kuongea kiukweli, acha nikupe maua yako Mke wangu, Unathamani kubwa katika maisha yangu kazi kubwa ya kututunza mimi na hawa wanangu siyo rahisi, kuishi vyema na wazazi wangu,kuwafurahisha mawifi na mashemeji kiukweli wewe ni mfano wakuigwa mwanamke na nusu

Sababu umeacha Furaha yako kwa ajili ya sie tuliokuzunguka tufurahi kwanza angalia picha inazungumza nawapenda sana dunia nayoishi pamoja na wewe ni zaidi ya pepo kiufupi asante Mungu kwa kunifanya wewe kuwa Mke wangu,wanangu nimewachagulia mama bora”






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags