Rema kujenga chuo cha muziki

Rema kujenga chuo cha muziki

Mkali wa Afrobeat kutoka nchini Nigeria Rema (23) ameripotiwa kuwa na mpango wa kuanzisha na kujenga chuo cha muziki Barani Africa.

Chuo hicho ambacho kinadaiwa kugaharimu N200 milioni kitaitwa ‘Rema Music Institute’ kinatarajiwa kutoa mafunzo madhubuti kutoka wa walimu wasomi ili kuleta mapinduzi katika tasnia ya muziki Barani Africa.

Rema kupitia mtandao wake wa X siku chache zilizopita ameweka wazi kuwa lengo la kufungua shule hiyo ya muziki ni kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na kum-sapoti katika muziki wake ambapo amepanga kukuza kizazi kijacho cha talata ya muziki, uvumbuzi, ubunifu kwa Bara zima na siyo Nigeria pekee.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags