Rema haofii kuacha muziki, Jina lake litaendelea kuishi

Rema haofii kuacha muziki, Jina lake litaendelea kuishi

Mwanamuziki wa #Afrobeat kutoka nchini #Nigeria #Rema ambaye anaendelea kutamba duniani kote amedai kuwa hata kama akiacha muziki leo basi jina lake litaendelea kuishi kwenye kitabu cha wakali wa #Afrobeat nchini humo.

Kufuatia mahojiano yake na jarida la #I-Dmagazine, #Rema alieleza kuwa anafahamu historia ya muziki huo na jina alilo jitengenezea.

“Sisemi nataka kuacha muziki, lakini nikisema nataka kuacha sasa hivi, jina langu bado litakuwa kwenye kitabu cha wakali wa #Afrobeats, ikiwa kama kutakuwa na kitabu hicho na litakuwa ukurasa wa mbele kabisa”

Ikumbukwe #Rema anaendelea kupeperusha bendera ya #Nigeria baada ya kutumbuiza katika usiku wa Tuzo za Ballon d’Or 2023 jijini Paris.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags