Refa wa Mauritania kuzihukumu Al ahly na Yanga

Refa wa Mauritania kuzihukumu Al ahly na Yanga

Abdel Aziz Mohamed Bouh kutoka Mauritania, ndiye refa aliyepangwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga na Al Ahly itakayochezwa Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

Yanga imekuwa na historia nzuri na refa huyo kwani ndiye alichezesha mechi kati yao na TP Mazembe ya hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita ambayo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-1, ushindi ambao uliweka hai matumaini yao ya kusonga mbele kwenye kundi lake.

Kumbukumbu zinaonesha kuwa timu za nyumbani zimekuwa na bahati na refa Bouh kwani katika mechi hizo 11 alizochezesha, ni michezo miwili tu ambayo wageni walipata ushindi huku wenyeji wakiibuka na ushindi mara saba mechi mbili zilimalizika kwa sare.

Ni refa ambaye amekuwa na bahati ya mabao kufungwa katika mechi anazochezesha kwani katika mechi hizo 11 alizoshika filimbi katika mashindano ya klabu Afrika, ni mchezo mmoja tu ambao ulimalizika kwa sare tasa.

Lakini sio tu Yanga bali hata Al Ahly nao imekuwa na bahati narefa huyo kwani imekutana naye mara moja na katika mechi hiyo, iliibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya CR Belouizdad.

Cc: Mwanaspoti
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags